Alhamisi 10 Septemba 2026 - 22:01
Iran Haitainamisha Kichwa Mbele ya Vitisho na Uonevu wa Mabavu / Tunahitaji Moyo wa Kijihadi Katika Mapambano ya Kiuchumi

Hawza/ Katibu wa Baraza la Walinzi amesema: Hatua madhubuti iliyochukuliwa na Vikosi vya Wanajeshi vya Iran katika kujibu uvamizi wa Marekani na kulenga maslahi pamoja na vifaa vyake, imeonesha kwamba Iran haina nia ya kuinamisha kichwa mbele ya uonevu na vitisho.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kutoka Tehran, Ayatullah Ahmad Jannati, Katibu wa Baraza la Walinzi, mwanzoni mwa kikao cha jana, Jumatano tarehe 18 Shahrivar 1405, cha Baraza hilo, huku akirejea kumbukumbu ya mwaka ya uasi wa tarehe 17 Shahrivar na ukandamizaji wa wananchi uliofanywa na utawala wa Pahlavi, amesema: Wananchi wa Iran kwa miaka mingi wamekuwa wakipambana dhidi ya madola ya kibeberu na wamegundua kwamba njia pekee ya kuzuia kutimia malengo ya watawala wa kibeberu ni muqawama.

Katibu wa Baraza la Walinzi, huku akirejea uvamizi wa hivi karibuni wa adui dhidi ya ardhi ya Iran na kulengwa meli za mafuta, amevishukuru Vikosi vya Wanajeshi vya Iran kwa jibu lao madhubuti na kusema: Hatua madhubuti iliyochukuliwa na Vikosi vya jeshi la Iran katika kujibu uvamizi wa Marekani na kulenga maslahi pamoja na vifaa vyake, imeonesha kwamba Iran haina nia ya kuinamisha kichwa mbele ya uonevu na vitisho.

Amesisitiza: Maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanapaswa kufahamu kwamba kila shinikizo na uvamizi utakabiliwa na jibu lililo imara zaidi.

Umuhimu wa kuamini uwezo wa ndani

Ayatullah Jannati pia ameashiria hatua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ya kutwaa kama ngawira manowari moja ya kisasa ya Marekani kuwa ni dhihirisho jingine la nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kuongeza: Nguvu hii imetokana na imani na inategemea elimu, taarifa, teknolojia, pamoja na uwezo wa kutambua na kukabiliana na zana za kisasa zaidi za adui.

Amesema: Mafanikio haya yanapaswa kuwa chanzo cha matumaini na kuongeza zaidi imani ya wananchi katika uwezo wa vijana na rasilimali za ndani za nchi.

Tunahitaji moyo wa kijihadi katika medani ya uchumi

Katibu wa Baraza la Walinzi, katika sehemu nyingine ya hotuba yake, akisisitiza umuhimu wa kulichukulia kwa uzito vita vya kiuchumi kama inavyofanywa katika medani ya kijeshi, amesema: Adui anajua kwamba ikiwa hataweza kuushinda Umma wa Iran kupitia vita na mashambulizi ya kijeshi, huenda akaingia kupitia njia ya shinikizo la kiuchumi na kufanya maisha ya wananchi kuwa magumu; hivyo, kukabiliana na vita hivi hakuwezi kufanyika kwa hotuba na nasaha pekee.

Ameendelea kusisitiza: Moyo uleule wa jihadi, harakati, kasi ya kuchukua hatua na uongozi wa kijeshi unaopatikana katika medani ya kijeshi, unapaswa pia kuonekana katika medani ya mapambano ya kiuchumi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha